Nyumba 2018-08-23T12:14:52+00:00
Two young people browsing the internet

Tuseme ukweli.

Lini ilikuwa mwisho wako wa kusoma maagizo na maelekezo kabla ya kujisajili katika mitandao ya jamii kabla ya kupata huduma yoyote?

Hatuwezi kulaumu. Ni rahisi kujipoteza katika misamiati ya sheria.

Lakini kusema kweli huwezi ukajua lipi ambalo laweza kupata kwa kubonyeza kidude kisemacho nishasoma na kuelewa masharti na maagizo. Hivi sasa ebu tafakari kitakacho fanyika wakati ambapo unasajili nambari yako ya kitambulisho, wakati unapiga kura na wakati unapolalamikia huduma za jamii.

Acha tuyajadili kwa kina.

Did you know that privacy is your human right?

Haki kwa faragha yako inaashiria kulindwa kwa data yako ya binafsi isiwekwe kwa umma bila kubali yako. Ni muhimu sana haki yako inapolindwa. Faragha ni kiini kikubwa kwa maisha ya binadamu yeyote pamoja na uhuru na haki wa ushirikiano na wa kujieleza.

“Sina lolote la kuficha!” 

Ni nini maana ya data ya binafsi?

Data ya binafsi inajihusisha zaidi na utumizi na utawala wa data ya binafsi. Hii yahusisha ukusanyaji, utumizi na usambazaji wa data yako ya binafsi na makampuni ama ata serikali.

Sisi sote tuna siri. Kubwa na ndogo.

Tafaraki haya, unapomweleza rafiki yako kuhusu siri fulani alafu rafikiyo anatumia ujumbe huo kukuhukumu ama zaidi anaenda kusamabaza kwa watu wengine ambao wanaenda kutumia siri yako kukuendesha.

Haya ndio yanayofanyika data yako ya faragha inapowafikia watu wengine bila kubali yako.

Man hiding computer screen
Citizen Engagement

Haki yako ya kidijitali inaathiri aje ushirika wako kama mwananchi?

Mara nyingi kura katika nchi za Afrika zimeharibika kutokana na uvamizi wa demokrasia kuanzia kwa vita na kutishiwa hadi kuibwa kwa kura.Wananchi kihistoria wamenyanganywa haki yao ya kujihusisha kwa siasa na uhuru wa kupata habari.Teknolojia imegeuza jinsi wananchi wanaweza jihusisha na mambo ya siasa kote barani.

Ingawaje kuna mwongezeko wa uthibithi wa utumiaji wa mtandao kama vile kuzimwa kwa mtandao na sheria mbaya kuhusu uhalifu mtandaoni.Kwa bahati mbaya nchi za afrika zinakosa mbinu hitajika kushirikisha wananchi na wengine wote katika njia za ufumulizi wa sheria hizo za mtandao na haki zao za kidigitali ambazo zinawaathiri moja kwa moja. Kwa mfano kura ambazo mnapiga huenda ikawa si ya siri, data yako ya afya hospitalini yawezekana hailindwi vikamilifu.

Lakina hatukosi uwezo kwa kuwa kwa kujua mengi ndiko twaweza linda na kupigania haki zetu vilivyo.

Jifunza mengi kuhusu tahadhari, ulinzi na usalama wa kidigitali hapa chini.

Man covering eyes of someone on their laptop
Man covering computer user's eyes
Woman's computer being monitored
Woman's computer being watched by cameras and spies
Man spamming and hacking
Man phishing information online