Surveillance 2018-09-06T11:09:16+00:00
Woman's computer being monitoredWoman's computer being watched by cameras and spies

Hii ni hali ambapo utumiaji wako wa mtandao unafuatiliwa na washirika wa kando kama vile watoaji wa huduma za mtandao,mashirika ya binafsi,serikali,waajiri,taasisi za upekuzi na hata watu wengine wa kawaida.

Kama tuonavyo katika sinema ndivyo ambavyo tunaangaliwa na vifaa vingine kwenye mtandao.

Ulinzi au ngojo yaweza tumiwa kuchunguza atari,kama vizuizi na kuchunguza visa vya wizi ingawaje yaweza pia tumiwa vibaya kuchunguza data ya faragha mtandaoni kwa kujinufaisha kisiasa na kiuchumi.

Madai ya hivi sasa kutokana na sakata ya kampuni ya Cambridge Analytica yanaonyesha kuwa Rais Uhuru Kenyatta alitumia matokeo ya ulinzi na ngojo ya mitandao ya kijamii kuafikia ujumbe wa kampeni zake kwa wapiga kura tofautu.Hii iliwezeshwa kwa ajili Facebook inafuatilia ushirika wako katika mitandao ya jamii na hivyo basi kubaini mienendo zako na hivyo basi ujumbe huo unatumika kubuni ujumbe mwengine unaoguzia vitu unavyovipenda na pia hisia zako.

Ulinzi una uzuri na ubaya wake lakini wapi ambapo tutabainisha haya? Wengine wanaona uzuri kama faida bila kuzingatia atari zake kwa uananchi.

Ulinzi na ngojo zaweza athiri uaminifu uliopo kati ya wanainchi na serikali na katika shughuli za uraia.

Taasisi ya ukusanyaji ushuru ya Uganda , ambayo ni ya serikali hivi majuzi imeelekeza benki zote za kibiashara kutoa habari kuhusu shughuli zote za akaunti zinazomilikiwa. Walieleza kwamba data kutoka kwa akaunti hizo zitawafaidi mno katika kazi yao.Kusambazwa kwa data hii bila nia muhimu ni kuvamia uhuru na haki ya faragha ya data ya wateja wao.Yaweza tajwa kama ulinzi na ngojo ya data ya faragha na kifedha ya wanainchi.

Man accessing information on a laptop
Woman in job interview having her Social Media profile scrutinized

Umbo lako katika mitandao ya kijamii. Ni ya kuaminika au taka?

Umbo lako katika mitandao ya kijamii. Ni ya kuaminika au taka?
Tafakari haya, kwamba unaenda kwa mahojiano ya kazi unayoitamani na kabla uingie pahala pa mahojiano ,mwajiri wako wa mbeleni ashatoa uamuzi au hukumu kutokana na umbo lako katika mitandao ya jamii.Wengi wa waajiri zaidi ya asilimia tisini wako watatafuta umbo lako katika mitandao ya jamii kabla au wakati wa mahojiano.

Yawezakuwa unawaamini watu mnaobadilishana umbo lako mtandaoni.Mitandao hii huweka rekodi ya kila kitu ukifanyacho humo na hivyo basi mtu anapopata njia kuingia kwa mtandaoni yako basi siri zako zote zitafichuliwa na kusambazwa.

Kando na mwajiri wako ,tafakari ingekuwa ni serikali yako.Inaweza tumia aje data yako ya faragha kukubagua katika huduma unazozipokea?Au kutoa adabu kwako kwa kushikilia maoni yako tofauti kwa utendakazi wao, kupambana na ufisadi au kukosekana kwa barabara?Walinzi wa haki za binadamu na wanaharakati wengine kwa mara nyingi wamekuwa waathiriwa wa unyanyasaji na mateso,kufungwa jela na hata kifo kwa sababu ya maoni waliyoyatoa.

Wafikiria nini?

Je ulinzi na ngoja inaboresha usalama wa wanainch?

Polisi na idara zengine zatumia mbinu tatanishi kufuatilia mawasiliano ya watu ambao wanadhaniwa kuwa hatari kwa usalama wa wengine kama vile wapinzani katika siasa na mbinu zengine za kawaida kama vile kupata rekodi ya mazungumzo bila kubali kutoka kwa watoaji huduma za mawasiliano.Utumiaji wa mbinu hizi za teknolojia zina madhara mbaya kwa uhuru wa mazungumzo na hivyo basi kuzuia maoni tofauti hasaa katika siasa kwa vile watu wataogopa kutengwa kando na kuadhibiwa.

Ni vigumu kuipa kibali ulinzi na ngoja hii kwa jina la usalama wa nchi kwa sababu nchi yafaa kutumia mbinu za kimataifa ya ujuzi kulinda wanainchi wake kutokana na harakati za magaidi.Hata baada ya mbinu hizi zote, wanawake kote Afrika wanaendelea kuwa waathiriwa wa visa vya uhalifu kama vile unyanyasaji wa kimapenzi na kuuliwa ionekanavyo hivi maajuzi mwaka wa 2017 katika eneo la Entebbe ambapo wanawake 23 waliuliwa na mhalifu bado yu huru.

Inaction to Crimes