Hii ni hali ambapo utumiaji wako wa mtandao unafuatiliwa na washirika wa kando kama vile watoaji wa huduma za mtandao,mashirika ya binafsi,serikali,waajiri,taasisi za upekuzi na hata watu wengine wa kawaida.
Kama tuonavyo katika sinema ndivyo ambavyo tunaangaliwa na vifaa vingine kwenye mtandao.
Ulinzi au ngojo yaweza tumiwa kuchunguza atari,kama vizuizi na kuchunguza visa vya wizi ingawaje yaweza pia tumiwa vibaya kuchunguza data ya faragha mtandaoni kwa kujinufaisha kisiasa na kiuchumi.
Madai ya hivi sasa kutokana na sakata ya kampuni ya Cambridge Analytica yanaonyesha kuwa Rais Uhuru Kenyatta alitumia matokeo ya ulinzi na ngojo ya mitandao ya kijamii kuafikia ujumbe wa kampeni zake kwa wapiga kura tofautu.Hii iliwezeshwa kwa ajili Facebook inafuatilia ushirika wako katika mitandao ya jamii na hivyo basi kubaini mienendo zako na hivyo basi ujumbe huo unatumika kubuni ujumbe mwengine unaoguzia vitu unavyovipenda na pia hisia zako.
Ulinzi una uzuri na ubaya wake lakini wapi ambapo tutabainisha haya? Wengine wanaona uzuri kama faida bila kuzingatia atari zake kwa uananchi.