Security 2018-09-06T09:49:02+00:00
Man spamming and hackingMan phishing information online

Kufuatia kuboreshwa kwa uafikiaji,kumekuwapo na pia ongezeko la uhalifu mtandaoni kama vile wizi,kukatwakatwa na wizi wa utambulisho.Uogofyo wa mtandao inaleta hasara kiuchumi kwa taifa la Uganda ambapo fedha bilioni UGX22 zapotea kila mwaka kulingana na ripoti ya Africa Cyber Security 2016.Baadhi ya sababu za uhalifu mtandaoni kuenea mno ni kuongezeka kwa taratibu na ujuzi wa wahalifu kwenye mtandao bila kusahau ukosefu wa maarifa na kanuni za kufuatwa kutoka kwa serikali na mashirika mengine.Hivi sasa jumuia ya Afrika Mashariki haina sheria kamili ya kulinda data ya faragha.Kuna tu mfumo wa sheria za uhalifu mtandaoni zilizobuniwa mwaka wa 2008.

Usalama unaongea zaidi jinsi data yako ya faragha inavyolindwa. Data ya faragha yaanzia kwa nywila hadi kwa kadi za mkopo na data ya binafsi. Je kunayo usalama wa ujumbe huu kwenye mtandao? Au wajua pale ambapo ujumbe huo umewekwa na ni nani anayoiona?

Usalama ni jambo kubwa kwa sababu data yako ya binafsi yaweza kutumiwa kufanya vitu mbaya kama vile kuiga, wizi na matumizi mengine mbaya.

Jambo kubwa la kiusalama katika jumuia ya Afrika Mashariki ni utapeli data ambapo wahalifu hutuma barua taka wakidai kuwa imetoka kwa maeneo tarajiwa ili kuwafanya watu kutoa data yao ya binafsi kama vile numbari ya kadi ya mkopo na nywila.

Data yako ipo kwenye soko la ulanguzi au magendo? Usalama wa data

Wakati ambapo kampuni kama Facebook wanapoendelea na ukusanyaji wa data yako ni vyema pia kutafakari matokeo ya mbeleni ya data ikusanywayo na serikali.Tayari twajua kwamba nchi kama India washaanza kusanya data kubwa iliyo na maana sana kuhusu wananchi ili kuwaweza kufuatilia kila kitu wafanyalo kuanzia ufanyikazi wao hasaa waajiriwa wa serikali hadi kutunzwa kwa akaunti za benki au mahusiano ya rununu.Vilevile China inatumia data kupima utendakazi wa wananchi wake zaidi hadi kuwapa alama za utendakazi wao.Ukiwa na alama ya chini huenda hata usiruhusiwe kutumia huduma kama usafiri wa kijamii au hata kuondoka nchini.Haya basi na iwapo una habari tofauti kando na jinsi serikali inavyoendeshwa au ungependa kuripoti mtu mfisadi?Utabahatisha kuwa alama yako huenda ikashuka.

Hii yamaanisha nini hasaa kwa haki za binadamu kama vile faragha ,kujieleza ,matembezi na mengineyo?Bila kuzingatia serikali,kanuni za data za kampuni zaweza pia changia katika matokea ya kisiasa.Katika Amerika mwaka wa 2016 na hapa Kenya mwaka wa 2017 tulijulishwa hadharani kuwa data yaweka kuwa na matukio kubwa kwa tabia ,pande za kisiasa na mifumo ya kisiasa.

Nini maana ya magazeti kidole?

Vipimo vya biolojia yahusisha upimaji na uchanganuzi wa fizikia za watu na tabia zao.Hii yaweza kutumia magazeti kidole,sauti,nyuso,retina na mienendo ya irisi,maumbo ya mikino,enenzi na ndewe.Vipimo vya biolojia vyako haviyafanani na mwengine yeyote.Data hii inatumika kwa utambulisho na kukutambulisha pia.Data kutoka kwa vipimo vya biolojia yaweza basi kulinda na kurahihisha miendendo yako inayohitaji kujitambulisha kama vile kupiga kura ,kuafikia huduma za umma na kadhalika.

Vipimo vya biolojia hutumika zaidi na serikali katika vitambulisho vya kitaifa,usajili wa upigaji kura na katika uhamisho.Mwaka wa 2016 tume ya uchaguzi ya Uganda ilitumia vipimo vya biologia kuhakikisha uhakiha wa wapiga kura kabla ya uchaguzi kufanyika.Vipimo vya biolojia hutumika na mashirika ya binadamu kusajili wakimbizi na pia kampuni za binafsi kama vile taasisi za kifedha.

Hivyo basi tatizo ni lipi?Pasipokuwepo na njia mwafaka na kali ya kulinda data katika maeneo kama vile teknolojia ya kushindwa kutambuliwa basi data yaweza fika kwa mikono mbaya virahisi.Hii yaweza kuelekeza kwa wizi,kutambuliwa vibaya na hata kunyimwa haki kushirika kwa miradi ya umma.Vipimo hivi pia zaweza ruhusu serikali na mashirika ya binafsi kufuata miondoko zako zote hata kuingilia haki yako ya uhuru wa binafsi.

Man providing biometric information

Wazo: vipimo vya biolojia ni rafiki au adui wetu wa siku zijazo?
Unyanyasaji mtandaoni ni nini?

Unyanyasaji mtandaoni ni nini?

Mwelekeo mkuu hivi maajuzi ni kunyanyaswa kwa wanawake.Wanaweke wengi wa Uganda wako mtandaoni hivi sasa ikilinganishwa na awali.Data ya faragha kama vile picha na video husambazwa mtandaoni bila kubali yao.Wanawake mara kadhaa ni waathiriwa wa unyanyasaji,ufuatiliaji na dhuluma mingi mtandaoni lakini kima cha uhasama huo mara nyingi huisha bila kuripotiwa.Kulingana na ripoti ya hivi majuzi kutoka kwa umoja wa mataifa(UN),dhuluma mtandaoni una viwango sawa na dhuluma za fizikia kwa wanawake.


Kuna aina mingi za uhalifu mtandaoni na wanawake mara nyingi huwa huathiriwa mno kama vile kufuatiliwa na kusambazwa kwa data yao ya binafsi bila kubali yao.Wanawake katika viti vya umaarufu na mvuto kama vile wabunge na wanahabari hudhulumiwa zaidi mtandaoni kwa nia ya kuzuia shauri na maoni yao kwa maswala yanayohusisha jamii.Wanawake mara kadhaa huamua kupuuza maoni hayo hivyo basi kudhibiti kushiriki kwao kwa midhahalo na hata kupuuza utumizi wa mitandao ya kijamii na kuwafanya washambulizi wao washindi.

Woman being harassed from her mobile phone

Hujuma na mateso mtandaoni
Hujuma mtandaoni ni utumizi wa vyombo vya electroniki vya mawasiliano kuwanyanyasa na kuwadhulumu watu kwa kutuma ujumbe wa kuwatisha. Hii yaweza husisha malipizi, tishio la vita, ujumbe wa unyanyasaji wa kijinsia, kumtoa mtu umaarufu na hivyo basi kuwashinda waathiriwa.

Kufuatiliwa mtandaoni
Kufuatiliwa mtandaoni ni pale ambapo mtu anatumia mtandao kwa mfululizo kwa nia ya kutishia na kutia mtu uoga. Hii kwa mara kadhaa hufanywa kupitia barua pepe, mitandao ya kijamii, ujumbe mfupi na njia zinginezo mtandaoni. Kufuatiliwa mtandaoni pia yaweza andamana na mifumo mengine ya kutekeleza uhalifu mtandaoni za zamani na hata nje ya mtandao.

Kusambaza data ya faragha mtandaoni bila kubali ya wamiliki
Huku sanasana ni kutafuta na kusambaza data ya faragha kama vile picha na video bila kuwa na idhini au kubali kutoka kwa wamiliki wa data iyo ili kuwadhulumu na kuathiri umaarufu wao. Mfano ni picha na video za uchi kusambazwa kwa mitandao ya kijamii na kulazimu wenyeji kuomba msamaha baada ya kudhulumiwa na kuaibishwa.

Wizi wa kufananishwa
Huu ni wizi ambapo mtu anatumia vitambulisho vya kujitambulisha bandia kama vile kitambulisho cha kitaifa au leseni ya uendeshaji gari ambavyo sivyo zake ili kujikufanya mtu mwengine ili kujinufaisha au ata kutekeleza wizi kwa niaba ya mhusika mwenyeji.

Lugha chochezi
Huku ni kumdhalimu mtu kwa kutumia maumbile au tabia wanazojitambulisha nazo kama vile ubaguzi wa rangi, dini, maumbile na maoni yao.

Usambazaji wa data ya faragha mtandaoni
Huku ni kueka na kusambaza data ya faragha na inayotambulisha mtu kwa mtandao kwa nia mbaya ya kujinufaisha na kuwanyanyasa wenyeji. Data hii ya faragha inakusudiwa kufikia umma hadharani kwa mfano kupitia mitandao ya kijamii, ujumbe mfupi na pia kupatana uso kwa uso.

Tanga
Hili ni tendo la fitina na utani kwa kuanzisha mazungumzo ya kuudhi mtu kwa kutuma ujumbe, picha na video kwenye mtandao ya kijamii pakiwa na nia ya kughadhabisha na uchokozi kuzua hisia mbalimbali au mazungumzo tofauti kando na ya kawaida.

Chenga
Huku ni kuingia kwa tarakilishi au mtandao wa mtu mwengine bila ruhusa yao na kufanya mageuzi kwa programu na maunzi ili kuafikia nia fulani ambayo haikusuudiwa na wamiliki. Chenga yaweza pia kufanywa ili kuafikia data kama vile nywila na rekodi nyenginezo.

A man shocked at his infected computer

Programu hasidi nautapeli data

Programu hasidi ni programu ambayo imetengenezwa kwa nia ya kuleta madhara na kuharibu au kuafikia programu zengine za tarakilishi huku utapeli data ni tendo la kutuma barua pepe ikifanywa kana kwamba imetoka kwenye mhusika halisi ile kuwadanganya watu kupeana data yao ya faragha kama nywila na nambari za kadi za mkopo.Hizi barua pepe huonekana kutoka kwa watu halisi unaowafahamu vyema.

Wanahabari,mawakili,wateteaji haki za binadamu na mashirika ya kijamii na hata raia wa kawaida wamekuwa waathiriwa wa chenga na utapeli data kutoka kwa wahuni ambao hujifanya wanawakilisha na kufanya na serikali.Mashambulizi haya yanaweza kusudiwa kupata nywila za barua pepe na mitandao ingine ya kijamii.

Ni vyema sana kujitahadhari unapotumia mtandao kutokana na magaidi hawa.Hakikisha kwamba nywila unayotumia zina uzito na zabadilishwa baada ya muda mfupi.

Una kusudio la kuboresha maarifa yako ya usalama mtandaoni? Basi tazama baadhi ya rasilimali ya washirika wetu.
Ulinzi au ngojo