Kuafikia habari
Uganda ilikuwa kati ya nchi za kwanza kubuni sheria ya uhuru wa kupata habari.Sehemu ya kuafikia taarifa katika katiba 2005 na baadae uhuru wa kuafikia habari na kanuni 2011.Hii inaashiria kuwa kila mwananchi bila kuzingatia lolote ana haki na uhuru wa kuaafikia habari kutoka kwa serikali au mashirika mengine yanayowakilisha serikali.Hii ilibuniwa ili kuhakikisha utumizi kamili,uwazi na uwajibikaji wa serikali ili kuwapa wananchi nafasi ya kujihusisha katika maamuzi yanayowaathiri moja kwa moja kama vile utoaji wa huduma.
Cha kusikitisha mno ni kuwa kando na mipango hii yote,kuafikia habari muhimu kwa wanachi bado ni changamoto kubwa kwa sababu kadhaa kwa mfano kutosoma sheria,mifumo mirefu na mengineyo.Kuna hitaji kubwa kwa bunge na wananchi kuhakikisha kuwa uafikiaji wa habari unatimizwa kwa kuwahimiza watu na mashirika mbalimbali,utumiaji wa teknolojia kupunguza harakati ,kuboresha maarifa na ujuzi wa takwimu.
Ushawai jaribu kuafikia data ya jamii?