Mara nyingi kura katika nchi za Afrika zimeharibika kutokana na uvamizi wa demokrasia kuanzia kwa vita na kutishiwa hadi kuibwa kwa kura.Wananchi kihistoria wamenyanganywa haki yao ya kujihusisha kwa siasa na uhuru wa kupata habari.Teknolojia imegeuza jinsi wananchi wanaweza jihusisha na mambo ya siasa kote barani.
Ingawaje kuna mwongezeko wa uthibithi wa utumiaji wa mtandao kama vile kuzimwa kwa mtandao na sheria mbaya kuhusu uhalifu mtandaoni.Kwa bahati mbaya nchi za afrika zinakosa mbinu hitajika kushirikisha wananchi na wengine wote katika njia za ufumulizi wa sheria hizo za mtandao na haki zao za kidigitali ambazo zinawaathiri moja kwa moja. Kwa mfano kura ambazo mnapiga huenda ikawa si ya siri, data yako ya afya hospitalini yawezekana hailindwi vikamilifu.
Lakina hatukosi uwezo kwa kuwa kwa kujua mengi ndiko twaweza linda na kupigania haki zetu vilivyo.
Jifunza mengi kuhusu tahadhari, ulinzi na usalama wa kidigitali hapa chini.